Subscribe
Find us on

News & Media

Foundation News

Ujumbe kutoka kwa Mheshimiwa Kofi Annan, Kwa niaba ya Jopo la Watu Mashuhuri wa Umoja wa Afrika kwa Watu wa Kenya

Nairobi

Tarehe 4 Machi 2013, Wakenya wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi wa kihistoria.

Kupitia uchaguzi huu, wa kwanza kufanyika chini ya katiba mpya, Wakenya watatumia fursa na haki yao kumchagua Rais ajaye ikiwa pamoja na viongozi wengine kwenye ngazi mbali mbali kuanzia ngazi za Mitaa, Kanda na hadi kitaifa.

Tarehe 4 Machi 2013, Wakenya wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi wa kihistoria.

Kupitia uchaguzi huu, wa kwanza kufanyika chini ya katiba mpya, Wakenya watatumia fursa na haki yao kumchagua Rais ajaye ikiwa pamoja na viongozi wengine kwenye ngazi mbali mbali kuanzia ngazi za Mitaa, Kanda na hadi kitaifa.

Kamwe kabla itakuwa watu wa Kenya kuwa na sauti zaidi katika jinsi nchi yao ni kukimbia.

Haya itakuwa uchaguzi wengi kabambe uliofanyika nchini Kenya na kuchukua nafasi katika wakati muhimu katika historia ya nchi. Hii itakuwa fursa ya kwanza ya kipekee itakayowawezesha Wananchi wa Kenya kutumia uhuru wao Kuwachagua viongozi wao katika kipindi hiki muhimu cha historia mpya ya Kenya.

Uchaguzi huu ni sehemu muhimu katika historia ya Kenya ukizingatia kwamba ni uchaguzi wa kwanza kufanyika kufuatia uchaguzi uliokuwa na matukio ya kusikitisha ya Mwaka 2007. Ni matumaini yetu kuwa Wakenya watatumia uchuguzi huu kuimarisha umoja wa kitaifa na kuzizika tofauti zao, zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2007. Huu ni wakati wa kutibu majeraha ya uchaguzi uliopita na kujenga mshikamamo wa kitaifa, na kujenga uchumi na Kenya mpya.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, misingi imara na madhubuti inayosimamia utawala wa sheria, haki za binadamu na amani imeendelea kujengwa na kuimarishwa. Hivi sasa Kenya ina moja ya katiba ambayo bora katika bara la Afrika, ambayo inatoa fursa ya kuboresha, kulinda na kuendeleaza jamii, uchumi,, na haki za kisiasa kwa wananchi wote ikiwa pamoja na kujenga miundombinu ya kitaasisi katika haya mabadiliko muhimu nchini Kenya.

Kwa upande wa mabadiliko ya ndani upande wa Sheria na Mahakama, Taasisi hiyo imejijengea na kujipatia heshima, ikiwa pamoja na kupata imani kutoka kwa wananchi wa Kenya katika kipindi hiki cha mpito na mabadiliko. Idara ya Mahakama ni muhimili muhimu, hivyo inapaswa kutekeleza majukumu yake ya kikatiba bila woga na bila kuingiliwa na kutekeleza majukumu yake chini ya Katiba mpya.

Wakenya wamejitoa mhanga na wamefanya kazi ngumu kufikia katika hatua ya sasa hivi, hivyo ni muhimu kuendelea kutumia fursa na kujenga nchi iliyo imara na yenye maendeleo kwa wote. Haya mafanikio yasingewezekana bila juhudi za wakenya wote katika kuhakikisha kuwa mabadiliko ya ndani yanafanikiwa. Hii isingwezekana kama Viongozi wa Kisiasa, Watumishi Serikalini, watu kutoka katika sekta ya binafsi, Viongozi wa Kidini, Asasi zisizo za Kiserikali, Makundi ya Akina mama na vyombo vya Habari. Jitihada hizi zimezaa matunda. Uchumi wa Kenya unaonyesha dalili za kukuwa vizuri na utakuwa na uwezo wa kuvutia Uwekezaji, kuongeza ajira mpya na kutoa fursa kwa wote.

Uchaguzi wa tarehe 04 Machi 20013, kama ukiwa huru, wa haki na wa amani utakuwa muhimu katika kuhamua hatima ya Kenya kuweza kufikia kiwango chake cha maendeleo.

Hivyo, Uchaguzi lazima uwe huru, wa haki na amani. Uchaguzi huu lazima ufuate misingi ya Utawala bora wa Kisheria. Lazima usimamiwe kwa uadilifu na maamuzi ya wakenya yaheshimiwe. Kwa kufanya hivyo, Wakenya wataweza kudumisha na kulinda umoja na mshikamano. Hata hivyo, vitisho, vurugu za uchaguzi na uhasama wa kikabila vinaweza kutumika vibaya na kuvuruga uchaguzi.

Wakenya bado wanakumbuka yaliyojiri katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2008. Kwa mazingira hayo, Kenya ipo njia panda kuelekea katika kujibomoa kama taifa. Kwa maana hiyo, matukio na vurugu za hivi karibuni ni dhahiri kwamba hatua muhimu zinapaswa kuchukuliwa kuzuia matukio kama hayo yasije kuturejeesha katika hali ya kutisha ya mwaka 2008.

Hivyo ninawaasa, Wakenya wote, kuchukuwa tahadhari na hatua muhimu, kuhakikisha kuwa yaliyojitokeza katika uchuguzi uliopita hayatajitokeza katika uchaguzi ujao. Jeshi la Polisi lina nafasi muhimu kuhakikisha usalama wa raia.

Ninafuraha na karibisha dhamira ya wagombea urais, kufanya kampeni za amani na kistaarabu, na kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na wa haki.

Viongozi wa kisiasa, kidini na kijamii, wakemee kwa nguvu zote lugha yeyote yanayoashiria kuwagawa na kuwachochea Wakenya. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ina wajibu wa kusimamia uadilifu. Wakenya wote wana wajibu wa kuhakikisha kuwa zoezi zima la uchaguzi linakuwa huru na haki. Viongozi wa kisiasa, vyama vya siasa, vyombo vya Ulinzi na Usalama, Vyombo vya Habari na Wakenya wote wana wajibu na jukumu la kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa salama na wa amani.

Matokeo ya Uchaguzi- Ulio Huru na wa Haki yakipatikana lazima yaheshimiwe, na kama yana pingamizi, basi utaratibu wa kisheria ya kuyapinga ufuatwe. Uchaguzi siyo mashindano ambayo mshindi anachukuwa kila kitu, na mshindani aliyeshidnwa na watu wake basi wanapigwa vita ya kuwadhoofisha. Kinachotakiwa, ni kwamba mchakato wa uchaguzi na matokeo yake, unamthibitisha mshindi na kumlinda aliyeshindwa. Uchaguzi ukisimamiwa vizuri unatoa fursa kwa kukuwa kwa demokrasia na kutatua matatizo kwa njia ya amani.

Hivyo ni muhimu kwa wakenya kuamini kuwa uchaguzi ujao utazaa serikali ambayo itafanya kazi kwa maslahi ya wakenya wote.

Wanajopo wenzangu, Benjamin Mkapa na Graça Machel,na mimi tunaamini kuwa Wakenya wanahitaji amani na utulivu katika uchaguzi ujao, na hivyo uchaguzi huyo utakidhi matarajio yao. Katika safari zetu za mara kwa mara za kuja Kenya tangu mwaka 2008, tulipata fursa ya kushirikiana na Wakenya kutaka kada mbali mbali. Wamekuwa wakiendelea kutukumbusha kuwa wanatarajia kujenga nchi iliyo bora na yenye mafanikio. Kenya na Watu wake wanastahili kupata heshima na fursa hiyo.

Tarehe 4 Machi 2013, Wakenya wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi wa kihistoria.

Kupitia uchaguzi huu, wa kwanza kufanyika chini ya katiba mpya, Wakenya watatumia fursa na haki yao kumchagua Rais ajaye ikiwa pamoja na viongozi wengine kwenye ngazi mbali mbali kuanzia ngazi za Mitaa, Kanda na hadi kitaifa.

Notes to Editors
Media Contact

For media inquiries please contact:

Declan O’Brien
Main: +41 22 919 75 57
E-mail: obrien@kofiannanfoundation.org